HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
SHULE YA SEKONDARI BITALE
Email: bitalesec@gmail.com; Facebook: Bitale Secondary School
Reg No. 1114; Exam No. S1336; Simu: 0625971687 / 0756438922 / 0672963963
S.L.P. 82, KIGOMA.
SHULE YA SEKONDARI BITALE
Email: bitalesec@gmail.com; Facebook: Bitale Secondary School
Reg No. 1114; Exam No. S1336; Simu: 0625971687 / 0756438922 / 0672963963
S.L.P. 82, KIGOMA.
SHERIA ZA SHULE
- Uwahi shuleni muda uliopangwa, uwepo muda wote wa masomo na wa kazi ukifuata ratiba ya shule ndani na nje ya darasa.
- Uheshimu bendera pamoja na wimbo wa taifa.
- Popote ulipo uwe na tabia njema, heshima na utiifu kwa walimu, wafanyakazi na majirani wa shule, wanafunzi wenzako na binadamu yeyote.
- Ukifikiwa au kukutana na mwalimu au mtu yeyote anayekuzidi umri usimame kumsalimia. Pia mpokee mzigo kama atakuwa nao.
- Uwe daima safi (mwili, nguo na vitu vyote unavyotumia).Usijirembe kwa kutia nywele dawa, usiache nywele ziwe ndefu, kujichora, kutia wanja, Usiache kucha ndefu wala kupaka rangi au hina.
- Usivae kofia, jaketi, viatu vya ghorofa wala mapambo yoyote (herini, bangili, mikufu n.k.).
Uvae daima sare ukiwa shuleni, ukitoka kwa shughuli za kishule, na ukienda hospitalini - Usionekane katika mazingira ya wasiwasi (klabu, kumbi za starehe, nyumba za wageni n.k.) wala kujihusisha na ulevi na uvutaji wa aina yoyote.
- Usiwe na urafiki wa kimapenzi na mtu yeyote unatakiwa kuzingatia masomo.
- Uthamini kazi za aina zote na kuzifanya kwa bidii, ukishirikiana na wenzako katika usafi na utunzaji wa mazingira.
- Ulinde mali yako binafsi na ya shule (majengo, madawati, vitabu na vifaa vingine utakavyopewa). Usitoe dawati nje ya jengo lake pasipo agizo au ruhusa.
- Utambue ni marufuku kuiba, kugombana, kupigana, kutumia lugha chafu, kuchonganisha, kuchochea vurugu na kufanya mgomo.
- Usitoroke shule, bali utoe taarifa kama utashindwa kuhudhuria masomo.
- Ukubali mamlaka ya wanafunzi viongozi katika kushauri, kuonya na hata kuadhibu kabla tatizo lako halijaufikia utawala wa shule
- Usikatae adhabu.
- Uwe msikivu na mtekelezaji wa maagizo na mashauri ya walimu.
- Ukamilishe kazi zote zinazotolewa na walimu kwa wakati unaotakiwa.
- Uwe mtulivu muda wote darasani, mwalimu awepo au asiwepo vilevile.
- Ushirikiane vema na walimu pamoja na wanafunzi wenzako ili kupata msaada wa kitaaluma.
- Utambue ni kosa kubwa kuibia, kusaidiwa au kusaidia katika mtihani wowote. Ujitahidi kufanya vizuri mitihani ya mara kwa mara
- Usiende nje bila ya ruhusa maalumu; ukienda kwenye ibada uvae sare na kurudi shuleni mara, bila ya kupitia sehemu nyingine.
- Usimpokee mgeni yeyote tofauti na walioandikwa na mzazi, wala nje ya siku za kutembelewa, tena upate kwanza ruhusa ya mkuu wa camp na usimuingize ndani ya camp.
- Uzingatie muda wa chakula.
- Kwa kosa la kukwepa mtihani wowote, na vilevile la kuibia, kusaidiwa au kusaidia wakati wa kuufanya, utaandikiwa alama sifuri (0%) katika matokeo yako.
- Kwa baadhi ya makosa utapewa kwanza maonyo mawili, ambayo yataandamana na adhabu shuleni na kudai uandike barua ya kukiri kosa na kuahidi hutalirudia.
- Kwa makosa makubwa zaidi hutapewa maonyo, bali utasimamishwa kwa siku au wiki kadhaa, kama si kufukuzwa shule.
- Ukipoteza au kuharibu kitabu au kitu chochote cha shule utatakiwa kununua kipya na kurejesha
- Hutarudishiwa vitu visivyotakiwa shuleni vikinyang’anywa na uongozi.