Tungo ni neno au kifungu cha maneno kinachoweza kutoa taarifa iliyokamili au isiyokamili.
Mfano: (a) Kaka anawinda ndege.
(b) Tunakwenda
(c) Wageni waliofika.
Vipengele vyote hivi ni tungo, ambapo kipengele (a) Kinatoa taarifa kamili na kina maneno zaidi ya moja. Kipengele (b) Kinatoa taarifa kamili japokuwa kina neno moja, na kipengele (c) Ni tungo isiyotoa taarifa kamili.
Vipashio vya Lugha
Vipashio vya lugha ni viungo mbalimbali vinavyowekwa pamoja katika mpangilio fulani kisarufi, kuunda lugha:- Sauti
- Mofimu
- Neno
- Sentensi
Aina za Maneno
- Nomino - majina, aina za nomino, uundaji wa nomino kutoka kwa maneno mengine, wingi
- Vitenzi - vitendo katika sentensi, aina za vitenzi, mnyambuliko wa vitenzi
- Viwakilishi - maneno yanayowakilisha nomino; aina za viwakilishi
- Vivumishi - aina za vivumishi k.v vivumishi vya sifa, n.k
- Vielezi - vielezi halisi, vielezi vya namna n.k
- Viunganishi - a-unganifu, kuonyesha tofauti, sababu, sehemu n.k
- Vihisishi - maneno ya kuonyesha hisia k.v hasira, mshangao n.k
- Vihusishi - uhusiano wa nomino na mazingira yake
- Kinyume - kinyume cha maneno mbalimbali
Muundo wa Maneno
- Sauti na Silabi - aina za sauti(konsonanti, vokali), silabi, matamshi
- Shadda na Kiimbo - mkazo katika maneno, kiimbo(intonation)
- Viambishi - maana na aina za viambishi, uainishaji
- Mofimu - mofimo huru, mofimu tegemezi
- Viungo - Matumizi ya viungo k.v KWA, KU, JI, MA, NI, NA n.k
Upatanisho wa Maneno
- Ngeli - ngeli mbalimbali za Kiswahili k.v A-WA, KI-VI n.k
- Umoja na Wingi - wingi/umoja wa nomino, sentensi n.k
- Ukubwa na Udogo - onyesha ukubwa/udogo wa neno au sentensi
- Nyakati na Hali - nyakati(uliopita, uliopo, ujao, n.k), NGE, NGALI,
- Kukanusha - kukanusha sentensi katika hali na nyakati mbalimbali
Sentensi
- Aina za Sentensi - changamano, ambatano n.k
- Uchanganuzi wa Sentensi - kikundi nomino, kikundi tenzi n.k
- Virai na Vishazi - aina za virai, kishazi huru, kishazi tegemezi
- Shamirisho na Chagizo - shamirisho yamwa, kitondo n.k
- Uakifishaji - alama za kuakifisha k.v swali(?), kikomo(.) n.k