UTANGULIZI:
Sarufi ni sheri, kanuni na taratibu zinazopaswa kufatwa katika lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni zake. Sarufi ni kupanga maneno kwa ufasaha. Katika sarufi tunazingatia sauti (Utamkaji), aina za maneno, upatanisho wa maneno kisarufi pamoja na muundo wa sentensi za kiswahili.
NGELI ZA NOMINO
Neno ngeli maana yake ni aina au kundi. Hivyo ngeli ni vikundi vya majina ya kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka au kupanga nomino katika makundi yenye nomino zinazofanana. Ngeli huundwa kwa kuunganisha viambishi viwakilishi vya nomino.
Kwa mfano, neno kitabu. Tunasema, "Kitabu kimepotea - Vitabu vimepotea."
Kwa kuunganisha kiambishi "KI"(umoja) na VI(wingi), tunapata ngeli ya KI-VI. Ni muhimu kusisitiza kwamba tunazingatia viambishi, wala si silabi ya kwanza.Hivyo basi, maneno yasioyoanza kwa KI-VI kama vile chama -vyama yatakuwa katika ngeli ya KI-VI kwa kuwa yanachukua kiambishi KI => (Chama kimevunjwa - Vyama vimevunjwa.) Vivyo hivyo, kunayo majina yanayoanza kwa KI-VI yasiyokuwa katika ngeli ya KI-VI
maadam yanachukua viambishi tofauti. k.v: kijana => A-WA (kijana amefika- vijana wamefika).
Tumekuandalia sehemu tatu na maelezo yake kukupa mukhtasari wa ngeli zote za Kiswahili na jinsi baadhi ya maneno/viambishi vinavyobadilika kutoka ngeli moja hadi nyingine.
a) Sehemu ya kwanza inakupatia ngeli, maelezo yake, na mifano ya majina:
NGELI | MAELEZO | ||
| Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai k.v watu, wanyama, ndege, wadudu, miungu, malaika n.k Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwa sauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hata hivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti. | ||
Mfano: mtu - watu | |||
KI - VI | Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo. k.v kitoto. Mfano: Kitu - Vitu | ||
LI-YA | Hujumuisha majina ya vitu visivyo hai pamoja na yale ya ukubwa k.v jitu. Majina yake huchukua miundo mbalimbali. Baadhi yake huchukua muundo wa JI-MA (jicho-macho), lakini yanaweza kuanza kwa herufi yoyote. Kwa wingi, majina haya huanza kwa MA- au ME-. Mfano: Jani - Majani | ||
U-I | Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI(wingi). Mfano: Mti - Miti | ||
U-ZI | Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/' k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa. Mfano: Ukuta - Kuta | ||
I-ZI
Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini
huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi). Mengi
yake huanza kwa sauti /u/, /ng/, /ny/, /mb/, n.k Mfano: nyumba - nyumba
U-YA
Ni majina machache mno yanayochukua kiambishi U(umoja) na YA(wingi). Mfano: uyoga - mayoga
YA-YA
Hii ni ngeli ya vitu visivyoweza kuhesabika (nomino za wingi). Hayana umoja. Mengi ya majina haya huanza kwa MA- lakini yanaweza kuchukua muundo wowote. Mfano: maji
I-I
Ni ngeli ya majina ya wingi ambayo huchukua kiambishi I- kwa umoja na pia kwa wingi. Majina haya hayana muundo maalum. Mfano: sukari
U-U
Majina ya nomino za wingi yanayoanza kwa sauti /u/ au /m/. Hayana wingi. Mfano: unga
PA-PA
Ni ngeli ya mahali/pahali - maalum. Mfano: mahali pale
KU-KU
Ngeli ya mahali - kwa ujumla. Aidha, hujumuisha nomino za kitenzi-jina. Mfano: uwanjani
MU-MU
Ngeli ya mahali - ndani. Mfano: shimoni
b) Sehemu ya pili inaangazia jinsi ngeli mbalimbali zinavyotumia "a-nganifu", viashiria na viashiria visisitizi.